Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mteja alienunua mkate wenye tobo kulipwa fidia

WhatsApp Image 2021 05 26 At 14.32.31 660x400.jpeg Mteja alienunua mkate wenye tobo kulipwa fidia

Thu, 27 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Kampuni ya Mini Bakeries LTD ya nchini Kenya imeahidi kumlipa fidia mteja aliyelalamika kupitia mtandao wa twitter kwamba alinunua mkate na kukuta kuanzia kipande cha kwanza hadi cha mwisho vina tobo katikati.

Kampuni hiyo ambayo inazalisha mikate ya Supa Loaf, licha ya kumuomba msamaha mteja wake huyo aliyedai kuwa ni mtumiaji wa mkate wa muda mrefu lakini bado haijabainisha itamfidia nini na kwa kiasi gani.

Kupitia ukurasa wa twitter wa Supa Loaf wamendika hivi, “Habari Kellyinyani tumeiona tweet yako, tunaomba radhi pia tunaomba utuandikie anwani ya makazi yako na mawasiliano yako kupitia DM ili tuweze kukulipa fidia”.

TAZAMA MSAFARA WA MWANA WA KIFALME ULIVYOINGIA IKULU AKIKUTANA NA RAIS SAMIA

Chanzo: millardayo.com