Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtanzania aingia fainali mashindano ya Tehama ya dunia ya Huawei

E8047ace1ac15bd1db71dc1483379b05 Mtanzania aingia fainali mashindano ya Tehama ya dunia ya Huawei

Mon, 14 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WANAFUNZI wa Tanzania ni miongoni mwa washiriki wa fainali za Mashindano ya kimataifa ya Teknolojia ya Habarina Mawasiliano (TEHAMA) kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara yanayoandaliwa na Huawei chini ya kaulimbiu ya “Connectivity, Glory, Future”.

Kwa mwaka jana wanafunzi kutoka Tanzania na Nigeria walikuwa washindi wa jumla katika shindano hilo na hivyo kuwakilisha ukanda huo katika mashindano ya dunia.

Shindano hilo limezinduliwa jijini Johannesburg, Afrika Kusini jana katika hafla iliyofanyika kwa njia ya mtandao.

Shindano hilo linaaminika kuwa ndiyo kubwa zaidi la aina yake barani Afrika kwa kushirikisha nchi 14 na kuhushisha wanafunzi zaidi ya 50,000. Shindano hilo kwa mwaka huu limeshirikisha zaidi ya nchi 70 na kushindanisha wanafunzi 150,000 kutoka vyuo zaidi ya 2,000.

Tangu kuzinduliwa kwake miaka mitano iliyopita, Shindano la TEHAMA la Huawei limeendelea kukua na kuwa shindano kubwa zaidi la TEHAMA barani Afrika.

Katika uzinduzi uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya mawasiliano, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO) pamoja na wanafunzi, Makamu Rais wa Huawei Afrika Kusini, Liao Yong alielezea umuhimu wa mawasiliano katika zama za kutokusogeleana.

“Utofauti katika mapokeo ya kidigitali unazidi kuongezeka katika kipindi hiki ambacho dunia imekumbwa na janga la Covid-19. Wakati watu wanapojisomea na kufanya kazi mtandaoni, wale wenye changamoto za kidigitali wanaathirika zaidi,”alisema Liao.

Katika semina ya mtandaoni iliyoandaliwa na Unesco hivi karibuni ,ilibainishwa kuwa miundombinu ya kidigitali ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazokabili sekta ya elimu ya juu barani Afrika.

“Kufanya shindano hili mtandaoni kwa kipindi hiki kuna thamani ya kipekee, inaonesha kwamba Huawei kama waasisi wa miundombinu ya kidigitali Afrika pia tuko makini na mkakati wetu wa kuwekeza kwenye vipaji.

Mkakati unajumuisha kuwafundisha wataalamu wa Tehama kidigitali, kuhamasisha na kuwawezesha wanafunzi wa Tehama na kuongeza uelewa wa Tehama kwa watu wa kawaida,”alisema.

Kampuni ya Huawei imewekeza zaidi katika kujiandaa na mashindano hayo kwa kufanya maonesho kwenye vyuo 300, katika nchi 14 za Kusini mwa Jangwa la Sahara na jumla ya wanafunzi 50,000 watashiriki.

Mafunzo kuhusu mashindano haya yamesaidia zaidi ya wanafunzi 300 kupata nafasi za kazi. Mwanafunzi wa Tehama wa Tanzania, Emanuel Chaula alisema: “Tulifanya kazi kwa bidii kama timu kwa sababu tulitaka kutumia fursa hiyo kusafiri kwenda China kushindana katika fainali za ulimwengu mzima.

Tulitaka kuonesha Afrika na ulimwengu kuwa Tanzania ni mdau mkubwa wa Tehama na tunataka kuwa sehemu ya ukuaji huo katika nchi yetu”.

Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi, Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Kimataifa ya Elimu ya Unesco, Ydo Yao, aliipongeza Huawei kwa kuchukua jukumu la mfano kuunga mkono mipango inayounda, kubuni na kutoa ustadi wa Tehama kwa bara la Afrika.

Pamoja na kampeni kadhaa za mfumo wa ikolojia ya vipaji Kusini mwa Jangwa la Sahara, yakiwemo mashindano ya Tehama, Huawei inatarajia kufundisha zaidi ya wataalamu 700,000 wa Tehama ifikapo 2023.

Lengo ni kuziba pengo la ujuzi wa Tehama, kuendeleza mabadiliko ya kidigitali kwa viwanda, kuileta digitali kwa kila mtu, nyumba na shirika kwa ulimwengu uliounganishwa kikami

Chanzo: habarileo.co.tz