Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtangazaji wa zamani wa Radio ateuliwa kugombea Urais Msumbiji

Fdsresd Mtangazaji wa zamani wa Radio ateuliwa kugombea Urais Msumbiji

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Inhambane na Mtangazaji wa zamani wa Radio, Daniel Chapo ndiye aliyeteuliwa na Chama kilichopo Madarakani nchini Msumbiji kukiwakilisha katika uchaguzi mkuu ujao.

Chama cha Frelimo kimemteua Daniel Chapo kukiwakilisha katika uchaguzi wa mwezi Oktoba 2024 baada ya Rais aliyepo Madarakani Felipe Nyusi kusema kuwa hatawania Urais kwa muhula wa tatu.

Wanachama 250 wa Kamati Kuu ya Frelimo walihitaji siku mbili za mjadala na kura kadhaa kuamua kati ya wagombea wanne katika kinyang’anyiro hicho.

Rais Filipe Nyusi alitoa wito kwa Frelimo kumuunga mkono Daniel Chapo kuelekea katika uchaguzi na kumtaka mgombea kujiandaa katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live