Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtangazaji Maina Kageni aashiria anapanga kumuoa Ciru wa Kinuthia

C7953d2078448c9e Mtangazaji Maina Kageni aashiria anapanga kumuoa Ciru wa Kinuthia

Wed, 28 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mtangazaji Maina Kageni alimtambulisha Ciru wa Kinuthia kwa mashabiki wake Julai 14 akiwa likizoni nchini MarekaniMaina alisema Ciru ni rafiki wake wa karibu lakini hajaamua iwapo atamuoa kwa sababu anaogopa ndoaMashabiki wake akiwemo mchekeshaji Churchill wamekuwa wakimshinikiza amuoe Ciru kwa sababu ni mwanamke mrembo Mtangazaji maarufu wa stesheni ya redio ya Classic 105 Maina Kageni amerejea nchini kutoka Marekani ambapo amekuwa likizoni kwa majuma kadhaa.

Baadhi ya mashabiki wake wamekuwa wakimsihi Maina amuoe mrembo huyo lakini amekuwa akisema kwamba anaogopa ndoa licha ya kuwapenda wanawake.

Aidha, kupitia mitandao ya kijamii, Maina amefichua kwamba amepata penzi la dhati na hivi karibuni atakuwa anamuoa Ciru.

Mtangazaji huyo pia alifichua kwamba Ciru atakuwa anakuja Kenya mwenzi wa Agosti na iwapo mambo yatakuwa shwari, atafunga naye pingi za maisha.



Read also

Mbunge Rigathi Gachagua Aachiliwa kwa Dhamana ya KSh 12 Millioni

Maina alimtambulisha Ciru kwa mashabiki wake Julai 14 akiwa mjini Miami Marekani ila alimtaja kama rafiki wa karibu sio mpenzi.

Kwa kuwa amekuwa akishinikizwa kuoa, mtangazaji huyo amesema kwamba yuko tayari kumuoa Ciru ambaye atatua nchini mwezi ujao kutoka Marekani.

Mchekeshaji Churchill ni miongoni mwa Wakenya ambao wamekuwa wakimshinikiza Maina kuoa ikizingatiwa umri wake umeonga sana.

Maina amekuwa nchini Marekani kwa majuma kadhaa baada ya kujivinjari kwa wiki kadhaa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke