Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtangaza nia nchini Kenya Kuruhusu Bangi

Wajacko Prof Wajackoyah akiwa katika moja ya mahojiano na kituo cha televisheni

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Professor wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Nairobi, George Wajackoyah ametangaza nia ya kugombea Urais wa Kenya kwenye Uchaguzi ujao wa August 09 mwaka huu huku akisema akichaguliwa atahalalisha matumizi ya bangi Kenya ili kukuza uchumi wa Kenya "Nitakuwa Rais wa kwanza Afrika kuhalalisha bangi sijali wapiga kura wataonaje ila huu ni uamuzi sahihi"

Prof. George amesema ana shamba nchini Marekani kwa sasa na anajiandaa kulima bangi "Tunahitaji kutengeneza fursa za ajira kwa Watu wetu na kulima bangi kutafanikisha hili, shida yetu tuna mawazo hasi ukienda Denmark wanatumia bangi kwa matumizi ya dawa"

"Baadhi ya Viongozi wanapinga bangi wakisema ni mbaya wakati Viongozi haohao wanaiba mali za Umma na kujinufaisha kwa jasho la Watu masikini, wengine wakifanya mabaya unakuwa wa kwanza kuwanyooshea vidole wakati wewe mwenyewe unafanya mabaya tunatakiwa kupiga hatua"

Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Kenya imeiweka bangi kwenye orodha ya dawa za kulevya na yoyote anayekamatwa akilima, kuuza au kutumia bangi anaweza kufungwa jela kwa miaka isiyopungua 20.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live