Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtandao wa intaneti waripotiwa kupotea katika mataifa kadhaa ya Afrika

Mtandao Wa Intaneti Waripotiwa Kupotea Katika Mataifa Kadhaa Ya Afrika Mtandao wa intaneti waripotiwa kupotea katika mataifa kadhaa ya Afrika

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Usumbufu mkubwa wa mtandao umeripotiwa katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Mtandao wa intaneti umeripotiwa kukatika katika nchi kadhaa zikiwemo Afrika Kusini, Nigeria, Ivory Coast, Liberia, Ghana na Burkina Faso.

Kilichosababisha nyaya za kusambaza huduma hiyo kushindwa kufanya hakijabainishwa.

"Inaonekana kuna usumbufu wa mtandao, unaoathiri kutoka kaskazini hadi kusini mwa Afrika," ilisema Cloudflare Radar, ambayo inatoa taarifa juu ya miunganisho ya mtandao.

Kasi ya muunganisho wa intaneti nchini Ivory Coast ulipungua hadi karibu 4% Alhamisi asubuhi, kulingana na Netblocks, ambayo inafuatilia usalama wa mtandao na muunganisho wa intaneti.

Nchini Liberia kasi ya muunganisho wakati mmoja ilishuka hadi 17% wakati Benin ilikuwa 14% na Ghana 25%, Netblocks ilisema.

Nchini Afrika Kusini, Vodacom ilisema kuwa "wateja kwa sasa wanakumbana na matatizo ya muunganisho wa mara kwa mara kutokana na kukatika kwa nyaya nyingi chini ya bahari".

Chanzo: Bbc