Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtalii auawa Afrika Kusini

Mauaji KMNJRO Mtalii auawa Afrika Kusini

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Afrika Kusini wanachunguza mauaji ya mtalii mmoja raia wa Ujerumani ambaye amepoteza maisha katika jaribio la kuteka gari lililotokea mashariki mwa jimbo la Mpumalanga.

Raia huyo wa Ujerumani  alikua sehemu ya kundi la watalii wanne ambao pia ni raia wa Ujerumani waliofika nchini humo kutalii. 

Tukio hilo limetokea jumatatu ya jana jioni wakati wajerumani hao walipokua wanaelekea kwenye vyumba vya mapumziko wakitokea hifadhi ya Taifa ya nchi hiyo ya  Kruger .

Kundi la wahalifu linasemekana kuwaamrisha watalii waliokuwemo kwenye gari hilo kufungua milango ya gari lao , lakini dereva alifunga milango yote ambapo mmoja wa wahalifu alifyatua risasi kupitia dirishani na kumuua mtalii huyo papo hapo.

Baada ya tukio hilo kundi hilo la wahalifu lilitokomea bila kuchukua chochote , ambapo mkuu wapolisi wa eneo hilo Bw.Semakaleng Daphney Manamela  ameliita tukio hilo kuwa ni la kikatili sana. 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live