Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtahiniwa wa KCPE kaunti ya Nyandarua aafariki dunia akijifungua

9cbc7d0822499957 Mtahiniwa wa KCPE kaunti ya Nyandarua aafariki dunia akijifungua

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kamishna wa kaunti ya Nyandarua Benson Leparmorijpo alisema mwanafunzi huyo alifakiri dunia kutokana na kuvuja damu nyingi

- Mtahiniwa alikuwa tayari amefikishwa katika zahanati ya Pesi baada ya kuhisi uchungu wa uzazi wakati mtihani wa somo la Sayansi ulipoanza

- Mwili wa mwendazake sasa umehifadhiwa katika mochuari ya hospitali ya Nyahururu ukisubiri kufanyiwa upasuaji

Mtahiniwa wa darasa la nane kaunti ya Nyandarua ameaga dunia dakika chache baada ya kujifungua.

Mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma katika shule ya Pesi eneo la Abadares, alihisi uchungu wa uzazi dakika chache kabla ya mtihani wa somo la sayansi kuanza.

Kulingana na taarifa tuliyoipokea hapa TUKO.co.ke, mwanafunzi huyo alijifungua salama lakini akapungukiwa nguvu baadaye.

Akidhibithisha kisa hicho, kamshina wa kaunti hiyo Benson Leparmorijpo alisema mwanafunzi huyo alifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi.

Mwili wa mwendazake sasa umehifadhiwa katika mochuari ya hospitali ya Nyahururu ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

Kwenye habari zingine, mtahiniwa mwingine katika shule ya msingi ya Oyola kaunti ya Kisumu alijifungua vema mtoto wa kiume Jumatatu, Machi 22 wakati akifanya somo la hisabati.

Kwa sasa yuko katika hospitali ya kimishonari ya St. Elizabeth Chiga ambapo anafanyia mtihani wake.

Mitihani ya kitaifa ilianza rasmi Jumatatu, Machi 22 na inatarajiwa kukamilika Jumatano Machi 24.

Zaidi ya watahiniwa milioni moja kote nchini wanatarajiwa kufanya mtihani wa KCPE chini ya masharti makali ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya COVID-19.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke