Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtahiniwa bora KCSE 2020 asema masomo mtandaoni ya Babu Owino yalimsaidia

4052727edc0bcb89 Mtahiniwa bora KCSE 2020 asema masomo mtandaoni ya Babu Owino yalimsaidia

Tue, 18 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Simiyu Robison Wanjala alisema masomo mtandaoni ambayo Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino aliendesha hayakuwa ya bure

- Simiyu alisema masomo hayo yalimsaidia kukabiliana na mtihani wa KCSE

- Alimshukuru mbunge huyo kwa kuwafunza watahiniwa Kemia na Hesabu

Mtahiniwa bora katika Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) 2020 amemshukuru Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino kwa kazi nzuri aliyofanya kuwasaidia wanafunzi kujiandaa kwa mtihani huo.

Simiyu Robinson Wanjala kutoka Shule ya Murang'a High, ambaye aliibuka mwanafunzi bora na alama ya A, alisema masomo ya mtandaoni ambayo Mbunge huyo aliendesha hayakuwa ya bure

"Ningependa kumshukuru Mheshimiwa Babu Owuno kwa masomo ya mtandaoni ambayo alikuwa anafanya. Mimi binafasi nilifaidika na masomo hayo. Nilijifunza mambo mengi ambayo nilifanya," alisema.

Mwanafunzi huyo mwerevu alisema Owino aliwasaidia kujiandaa kwa somo la Kemia na Hisabati akiongezea kuwa watahiniwa wengine wanaweza pia kushuhudia.

Simiyu pia alimshukuru Babu kwa kutenga muda kutoka kwa ratiba yake yenye shughuli nyingi tangu janga la COVID-19 kuathiri shughuli za masomo.

Mnamo 2020 Babu aliwaomba watahiniwa wote wa KCSE kufuatilia masomo yake mtandaoni Ijumaa, Mei 1, kwa somo la Hesabu.

Mbunge huyo alitoa mwongozo katika maswali kuu kwenye somo hilo mubashara kwenye Facebook.

Na ni dhahiri kwamba masomo hayo yalizaa matunda.

Katika matokeo yaliyotangazwa Jumatatu, mei 10, Simuyu Robinson Wanjala wa Shule ya Upili ya Murang'a ndiye aliyeibuka wa kwanza na alama ya A na pointi 87.334.

Muriasi Rob Ongare kutoka Shule ya Alliance High aliibuka wa nne na alama 87.173, huku Mbugua Esther kutoka Shule ya Kenya High akimalizia orodha ya wanafunzi tano bora na A ya pointi 87.113.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke