Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtahiniwa afariki baada ya kujifungua

Mimba Mashuleniiii Mtahiniwa afariki baada ya kujifungua

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watahiniwa kadhaa wa kike wanaofanya mitihani ya kitaifa ya shule ya msingi, nchini Kneya wamejifungua, vyombo vya habari vya nchini homo vinaripoti.

Baadhi yao wamefaulu kuendelea na mitihani lakini siku ya Jumanne mwanafunzi wa miaka 19 ambaye alifariki baada ya kupata matatizo wakati kujifungua.

Velma Ochieng, mwanafunzi wa shule ya msingi huko Homa Bay, magharibi mwa Kenya, alifariki muda mfupi baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji.

Visa vya watahiniwa kufanya mitihani ua shule za msingi na sekondari wakiwa wajawazito zimekuwa zikishuhudiwa sana nchini Kenya.

Gavana wa kaunti ya Homa Bay alitaka uchunguzi ufanywe kubqini kilichosababisha kifo cha Velma.

"Tutaendeleza juhudi zetu kuhakikisha hakuna mama anayepoteza maisha wakati wa kujifungua haswa kama inawezekana," Gladys Wanga alisema.

Katika kaunti ya kusini-magharibi ya Narok wasichana 248 wajawazito ni miongoni mwa watahiniwa wanaofanya mitihani ya kitaifa.

Kamishna wa Kaunti Isaac Masinde alisema magari ya kubebea wagonjwa yamewekwa kwenye hali ya kusubiri iwapo yatahitajika kuwakimbiza watahiniwa hao wajawazito hospitalini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live