Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva atambulishwa Wydad Casablanca, apewa namba 11 na sio 27 kisaa?

E1B3AD3B 4BF8 4271 B3EA 921CB66ACA87 660x400.jpeg Msuva atambulishwa Wydad Casablanca, apewa namba 11 na sio 27 kisaa?

Mon, 7 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Mtanzania Simon Msuva jana alitambulishwa na klabu yake mpya ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco na kukabidhiwa jezi namba 11 na sio 27 kama tulivyomzoea au 12 anayoitumia timu ya taifa.

Msuva ameeleza amechukua jezi hiyo baada ya kukuta jezi namba 27 ina mtu lakini 11 ndio namba yenye historia nyuma ya pazia, Msuva amesema amechukua jezi namba 11 kama heshima kwa mchezaji wa zamani wa Simba SC Musa Mgosi ambaye aliwahi kumuona akiwa mtaani akicheza na kumwambia atafika mbali ana uwezo mkubwa sana.

Musa Mgosi

“Aliyefanya niipende zaidi namba 11 ni Musa Hassan Mgosi watanzania wengi labda walikuwa hawafahamu mimi shabiki mkubwa wa Mgosi, aliwahi kuniona Sinza kwenye mechi za mtaani nikicheza na timu ya mtaani kwake”

“Alisikia kuwa kuna kijana anaitwa Simon anajua sana mpira ndio akataka anione, alivyoniona kuna maneno akaniambia wewe kijana unajua sana mpira lazima utafika mbali na alinipa zawadi ya jezi yake namba 11 ya Simba nikawa naenda nayo kwenye Ndondo”>>>.Msuva

Chanzo: millardayo.com