Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva ampaisha Mgosi, Wydad

468a18d2a90a3ccff450206bbb9943f8 Msuva ampaisha Mgosi, Wydad

Mon, 7 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MCHEZAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ambaye juzi alitambulishwa na klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco amesema alichagua jezi namba 11 kumpa heshima mchezaji wa zamani wa Simba, Musa Mgosi.

Msuva alitoa kauli hiyo baada ya kutambulishwa na Wydad ambayo amesaini mkataba wa miaka minne akitokea Difaa El Jadida ya nchini humo.

Msuva alisema alichukua jezi hiyo baada ya kukuta namba 27 aliyozoea kuivaa ina mtu hivyo alichukua 11 kwa ajili ya kumpa heshima Mgosi ambaye aliwahi kumtabiria makubwa akiwa mdogo.

“Nimechukua jezi namba 11 kama heshima kwa mchezaji wa zamani wa Simba, Musa Mgosi ambaye alinitabiria kuwa nitafika mbali kwa kuwa nilikuwa na uwezo na nilikuwa najituma,”.

“Mgosi alisikia kuna kijana anaitwa Simon anajua sana mpira ndio akataka anione, alivyoniona akaniambia wewe kijana unajua sana mpira lazima utafika mbali na alinipa zawadi ya jezi yake namba 11 ya Simba nikawa naenda nayo kwenye ndondo,” alisema Msuva.

Msuva ambaye kabla kusajiliwa Yanga, alikuwa Moro United akiwa Difaa El Jadida alikuwa anavaa jezi namba 27 na kwenye kikosi cha Taifa Stars anavaa jezi namba 12.

Chanzo: habarileo.co.tz