Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msumbiji yashauri 'visu na mapanga’ vitumiwe katika vita dhidi ya wanamgambo

Wanamgambo Msumbiji yashauri 'visu na mapanga’ vitumiwe katika vita dhidi ya wanamgambo

Fri, 30 Sep 2022 Chanzo: BBC

Mkuu wa polisi wa Msumbiji amewataka wakazi katika ameneo yaliyoshambuliwa hivi karibuni na jihadi kasakazini mwa jimbo la Cabo Delgado kupambana na washambuliaji.

Ikatika mazungumzo na wakazi wa eneo hilo, Bernardino Rafael aliwataka watu kutumia njia zote zilizopo kukabiliana na wanamgambo hao na akatia wito kwa jamii kuweka ulinzi wao ili kujilinda.

“Sasa sio muda wa kukimbia. Ni muda wa kukabiliana. Na wakati )jihadi) wanapoingia katika uwanja kile tunachopaswa kukifanya ni kuwafukuza na kupambana nao kwa kidsu, panga au mkuki na halafu mmoja wenu anakimbilia kuwasiliana na vikosi vya usalama ili vijiunge na kuwafukuza mbali hawa jihadi,” alisema.

Aliuhakikishia umma kwamba wanamgambo wanasakwa na baadhi waliuawa wakati wa makabiliano ya silaha.

Katika wilaya ya Quissanga, raia, hususan vijana, waliomba wapewe silaha ili wasaidie kulinda ardhi yao dhidi ya uvamizi wa wapiganaji wa jihadi.

Mkuu huyo wa polisi aliwahakikishia kuwa wale wenye vigezo wataingizwa katika kikundi cha eneo – kinachoshirikiana na wanajeshi wa serikali na washirika wa kimataifa katika vita dhidi ya ugaidi.

Chanzo: BBC