Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msumbiji yaagizia kuku kutoka Brazil, Uturuki

KUKUU 0 Msumbiji yaagizia kuku kutoka Brazil, Uturuki

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msumbiji imetangaza kuwa, imeamua kuagiza kuku kutoka Brazil na Uturuki ili kupunguza uhaba wa nyama ya kuku baada ya Maputo kupiga marufuku kuingiza bidhaa hizo kutoka nchi jirani ya Afrika Kusini kutokana na kukumbwa na homa ya mafua ya ndege.

Akitangaza habari hiyo, Americo Conceicao, Mkurugenzi Taifa wa Maendeleo ya Mifugo katika Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Vijijini ya Msumbiji amesema: "Waagizaji wa bidhaa za kuku wa nchini Msumbiji wamepewa kibali cha kununua takriban tani 4,000 za kuku kutoka nchi mbili za Brazil na Uturuki na bidhaa hizo zinatarajiwa kuwasili nchini humo baada ya takriban mwezi mmoja."

Vile vile amesema: Wazalishaji wa ndani wanaweza pia kuagiza mayai ya kuanguliwa kutoka Brazili na Uturuki ili kuhakikisha mchakato wa uzalishaji wa kuku na bidhaa zake haukwami na hauzoroti nchini Msumbiji. Homa ya mafua ya ndege yailazimisha Msumbiji kupiga marufuku kuingiza kuku kutoka Afrika Kusini

Bei ya kuku na mayai imepanda nchini Msumbiji tangu serikali isitishe kuingiza kuku wiki iliyopita kutoka Afrika Kusini, ambapo mafua ya ndege, yaliyosababishwa na homa aina ya H5N8, H5N1, H5N2 na H7, yaligunduliwa katika majimbo ya Gauteng, North West, Western Cape na mikoa ya Mpumalanga, Free State, Kwazulu Natal na Eastern Cape.

Mwaka 2021, Msumbiji iliingiza nyama ya jamii ya ndege kutoka nje hasa kutoka Afrika Kusini yenye thamani ya dola milioini 45.6 za Kimarekani. Mwaka huo iliingiza kuku wenye thamani ya dola milioni 10.9 kutoka Afrika Kusini, milioni 7.18 kutoka Uholanzi, milioni 6.66 kutoka Brazil, na milioni 3.38 kutoka Poland, ukitoa maeneo mengine duniani.

Afrika Kusini imekumbwa na mripuko mbaya zaidi wa homa ya ndege, na kuwatia hasara wafugaji milioni saba wa kuku na jamii ya ndege wanaotaga mayai, ambao wanaunda asilimia 20 hadi 30 ya hifadhi yote ya wanyama wa aina hiyo nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live