Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msumbiji inapendekeza kupunguzwa kwa mishahara kwa maafisa wakuu

Msumbiji Inapendekeza Kupunguzwa Kwa Mishahara Kwa Maafisa Wakuu Msumbiji inapendekeza kupunguzwa kwa mishahara kwa maafisa wakuu

Fri, 26 May 2023 Chanzo: Bbc

Baraza la mawaziri la Msumbiji limeidhinisha mswada unaopendekeza kupunguzwa kwa mishahara ya mawaziri, manaibu waziri, makatibu wa majimbo na wabunge huku serikali ikikabiliana na mswada wa mishahara kupanda.

Waziri wa Fedha na Uchumi Max Tonela siku ya Alhamisi alisema pendekezo hilo pia lilikuwa linataka kushughulikia maswala ya mishahara ya wajumbe wa mabunge ya majimbo, ambayo alisema yanakinzana na kanuni za malipo ya haki.

Bw Tonela alisema baadhi ya mishahara yao ni ya juu zaidi kuliko ile inayolipwa watendaji wengine na wataalamu waliobobea.

Hakuonyesha kiasi cha kupunguzwa kilichopendekezwa.

Mapunguzo hayo ya mishahara hayatatumika kwa watumishi wa umma ambao mishahara yao ilirekebishwa chini ya Kiwango cha Malipo Pamoja (TSU) kilichoidhinishwa mwaka huu.

Hatua hiyo inajiri takriban wiki mbili baada ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF kuangazia haja ya serikali kupunguza matumizi ya mishahara ya umma.

Mswada wa mishahara utawasilishwa bungeni kwa mjadala kabla ya kupitishwa kuwa sheria.

Chanzo: Bbc