Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msumbiji : Watoto zaidi ya 70 hawajulikani walipo

Wanajihadii.png Msumbiji : Watoto zaidi ya 70 hawajulikani walipo

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watoto 70 hawajulikani walipo kufuatia mashambulio ya hivi karibuni ya wanajihadi wa kiislamu katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado nchini Msumbiji, mamlaka nchini humo zimesema.

Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama na wakazi wa êneo hilo, watoto hao walitenganishwa na família zao, huku maelfu ya raia wakiripotiwa kukimbilia kwenye jimbo jirani la Nampula.

Kuna hofu kuwa, huenda baadhi yao wametekwa nyara na wapiganaji hao wanaohusishwa na kundi la Islamic State.

Tukio hili limejiri baada ya hivi karibuni, kushuhudiwa tena ongezeko la vitendo vya mashambulio yanayofanywa na wanajihadi wa kiislamu, ambapo kwa mujibu wa shirika la kimataifa la madaktari wasio na mipaka, MSF watu zaidi ya laki 8 wamekimbia makazi yao tangu mwezi Januari mwaka huu.

Huu ni mwaka was aba sasa tangu wapiganaji wa Al Shaabab wenye uhusiano na Islamic State watatize usalama kwenye jimbo la Cabo De Gado lenye utajiri wa Gesi, vikosi vya Serikali vikisaidiwa na vile vya Rwanda kuwadhibitia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live