Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msumbiji: Mtanzania miongoni mwa watu 16 wanaotuhumiwa kuunga mkono ugaidi

Msumbiji: Mtanzania Miongoni Mwa Watu 16 Wanaotuhumiwa Kuunga Mkono Ugaidi Msumbiji: Mtanzania miongoni mwa watu 16 wanaotuhumiwa kuunga mkono ugaidi

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa Msumbiji imemtaja mwanamke Mtanzania miongoni mwa watu 16 walioshitakiwa kwa tuhuma za kuunga mkono harakati za wanamgambo kaskazini mwa Mkoa wa Cabo Delgado, shirika la habari la AIM liliripoti tarehe 19 Aprili.

Mwanamke pekee aliyejumuishwa katika orodha hiyo ni mkulima mwenye umri wa miaka 36 kutoka Tanzania ambaye inasemekana alijiunga na kundi la wanamgambo Oktoba 2020.

Baadhi ya washukiwa wengine ni wakulima, wavuvi au wafanyabiashara kutoka wilaya za Palma na Mocimboa da Praia, ambao wanatuhumiwa kushiriki katika mashambulizi ya kigaidi, kufadhili na kuwasajili wanachama wapya wa kundi la waasi.

Mmoja wa washukiwa hao alikuwa mwanamume ambaye aliripotiwa kuajiriwa na waasi kuwasakili vijana 50 kwa kuwaahidi dola 15,500 za Kimarekani kila mmoja, ripoti hiyo ilisema.

Mshukiwa mwingine ambaye ni mfanyabiashara ya vyakula, alikamatwa na bidhaa mbalimbali za wizi zikiwemo mahindi, unga, mchele na jenereta za umeme, ambazo zilikusudiwa kusambaza kambi za wapiganaji katika kisiwa cha Vamizi.

Chanzo: Bbc