Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msumbiji: Maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi yazimwa na polisi

Msumbiji Maandamano.png Msumbiji: Maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi yazimwa na polisi

Fri, 18 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vikosi vya usalama nchini Msumbiji, Jumatano ya wiki hii vimelazimika kutumia nguvu kuwatawanaya mamia wa wafuasi wa mgombea huru wa urais, Venancio Mondlane, ambaye anadai kushinda uchaguzi wa urais wa Oktoba 9.

Kwa mujibu wa video aliochapisha mtandaoni, Mondlane anadai kuwa vijana watatu walijeruhiwa kwa risasi, mmoja kati yao akijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi kwenye mguu.

Hata hivyo idadi ya walijeruhiwa haijathibitishwa huku polisi nao wakikosa kuthibitisha iwapo kulikuwa na majeruhi.

Mondlane pamoja na wafuasi wake waliandamana katika mji wa Kaskazini Mashariki wa Nampula, kupinga matokeo ya uchaguzi yaliotangazwa na mamlaka za uchaguzi ambapo chama tawala cha Frelimo kilipata ushindi wa asilimia 66 ya kura katika jimbo la Nampula ambalo ni la kwanza kwa ukubwa nchini Msumbiji na linatajwa kuwa ngome ya upinzani.

Mwaka uliopita, polisi mmoja aliuawa kwenye maandamano katika jimbo hilo baada ya chama cha Frelimo kutangazwa kushinda uchaguzi wa manispaa.

Siku ya Jumanne, mwanasheria mkuu wa serikali alimuonya Mondlane dhidi ya kujitangaza mshindi kabla ya matokeo rasmi kutolewa, akisema hatua hiyo huenda ikachochea vurugu na ni kinyume cha katiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live