Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msimamizi wa "Day Care" atuhumiwa kuwanyanyasa watoto Kingono

Teresia Wambui Kihagi Teresia Wambui

Thu, 3 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimamizi wa Kituo cha Malezi na Uangalizi wa Watoto (DayCare), Teresia Wambui ameshikiliwa kwa siku 21 akichunguzwa Afya Ya Akili baada ya kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kuwatumia Watoto wadogo kutengeneza Video za ngono

Alipofikishwa Mahakamani Oktoba 1, 2024, Mahakama iliambiwa kuwa alijaribu kuvunja simu yake ili kuharibu ushahidi, lakini alinyang’anywa na simu hiyo iliwasilishwa Mahakamani kwaajili ya uchunguzi

Aidha, Watoto waliokuwa katika kituo hicho wamerudishwa kwa Wazazi wao huku wakiendelea kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live