Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshukiwa wa kike akamatwa baada ya afande kufariki saa chache walipoachana

609f74ec51185c1d Mshukiwa wa kike akamatwa baada ya afande kufariki saa chache walipoachana

Mon, 26 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Lucy Chepkorir anazuiliwa kutokana na kifo cha afisa huyo na uchunguzi unasubiri matokeo ya upasuajiIliripotiwa kuwa konstebo Kurgat alikuwa ameenda kutembea kwa Chepkorir na saa chache baadaye akafariki duniaChepkorir alikuwa na kesi nyingine ya uvunjaji wa sheria na sasa kisa cha afisa huyo kimefanya amulikwe zaidiPolisi Nakuru wanachunguza tukio ambapo mmoja wao alifariki dunia saa chache baada ya kutoka katika nyumba ya kipusa fulani.

Kisa hicho kilitokea katika kituo cha polisi cha Olenguruone ambapo konstebo David Kurgat alifariki dunia saa chache baada ya kumtembelea Lucy Chepkorir.

Uchunguzi unasema Chepkorir ni mshukiwa katika kisa kingine cha uvunjaji wa sheria na sasa kisa cha afisa huyo kimemuweka pabaya pia.

OCPD wa Kuresoi Kusini Henry Nyaraga alidhibitisha kisa hicho Jumamosi Julai 24 na kusema Chepkorir atazuiliwa ili kusaidia katika uchunguzi wa kisa hicho.

Nyaraga alisema baada ya mshukiwa huyo kukamatwa atasubiri ripoti ya upasuaji ili kujua kilichommaliza afisa Kurgat.

Read also

Kipusa Akamatwa Baada ya Polisi Kuzimia na Kuaga Dunia Katika Nyumba Yake

Afisa huyo alikuwa akihudumu katika kituo cha Kiptagich ambapo wenzake wanasema alikuwa ni mtu mchapa kazi.

Haijabainika alikuwa amefika nyumbani kwa mshukiwa Chapkorir kufanya nini.

Kwingineko, ripoti ya upasuaji ya mfanyabiashara Peter Ndwiga aliyeuawa Juja na afisa Caroline Kangogo ilionyesha alifariki kutokana na kuvuja damu.

Hili lilitokana na jeraha la risasi aliyopigwa kichwani usiku alipokutana na Kangogo kwenye chumba cha anasa.

Katika ujumbe ambao Kangogo alaicha alipojitoa uhai, hakujutia kumuua Ndwiga akisema alikuwa amemlaghai fedha zake.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke