Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanariadha Agnes Tirop akamatwa

06d7e04e94be19e2 Mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanariadha Agnes Tirop akamatwa

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanariadha bingwa wa mbio za masafa marefu Agnes Tirop amekamatwa siku chache baada ya mwili wake kwenye nyumba yake eneo la Iten kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Maafisa wa Upelelezi wamefanikiwa kumkamata mshukiwa wa mauaji ya mwanariadha Agnes Tiprop Ibrahim Rotich aliamatwa Alhamisi, Oktoba 14 akiwa eneo la Changamwe akijaribu kutorokea nchi jirani.

Mshukiwa kwa sasa anafanyiwa uchunguzi kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.

Mwili wa Tirop ulipatikana ukiwa umelowa damu Jumatano, Oktoba 13 baada ya madai kuibuka kwamba alidungwa kisu na mpenzi wake Ibrahim Rotich kabla ya kutoroka.

Kulingana na ripoti kutoka kwa maafisa wa DCI, Rotich alikamatwa akiwa eneo la Changamwe akijaribu kutorokea nchi jirani.

" Kwa sasa mshukiwa anahojiwa na maafisa wa upelelezi kutoka kituo cha polisi cha Changamwe, anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji, " Ripoti ya DCI ilisoma.

Kulingana na kamanda mkuu wa polisi eneo la Pwani John Elungata, mshukiwa atasafirishwa hadi Nairobi kwa uchunguzi zaidi dhidi yake.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke