Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Mshukiwa mkuu' akamatwa baada ya miili kupatikana jalalani Kenya

'Mshukiwa Mkuu' Akamatwa Baada Ya Miili Kupatikana Jalalani Kenya.png 'Mshukiwa mkuu' akamatwa baada ya miili kupatikana jalalani Kenya

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Polisi nchini Kenya wamemkamata mwanamume ambaye wamemtaja kama "muuaji wa watu wengi" anayeshukiwa kuhusika na mauaji ya kutisha ya wanawake tisa ambao miili yao iliyokatwakatwa ilipatikana kwenye machimbo ambayo yanatumika kama jalala.

Polisi wanasema Jomaisi Khalisia, 33, alikiri kuwaua wanawake 42 tangu 2022, akiwemo mkewe .

Mshukiwa alikamatwa katika baa mapema Jumatatu asubuhi alipokuwa akitazama fainali ya Euro.

Kumekuwa na mshtuko na ghadhabu nchini Kenya tangu maiti ya kwanza ya miili kupatikana siku ya Ijumaa katika mji mkuu, Nairobi.

"[Ali]kiri kuwarubuni, kuwaua na kutupa miili ya wanawake 42 katika eneo hilo la taka .Wote waliuawa kati ya 2022 na hivi majuzi Alhamisi," alisema Mohamed Amin, mkuu idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Alisema wamepata ushahidi muhimu katika nyumba ya mtuhumiwa, zikiwemo simu 10, tarakilishi bebe , panga, vitambulisho na mavazi ya kike.

Chanzo: Bbc