Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshukiwa mauaji ya kimbari ya Rwanda akamatwa tena Afrika Kusini

Mshukiwa Mauaji Ya Kimbari Ya Rwanda Akamatwa Tena Afrika Kusini Mshukiwa mauaji ya kimbari ya Rwanda akamatwa tena Afrika Kusini

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda Fulgence Kayishema, ambaye amekuwa akizuiliwa nchini Afrika Kusini, amekamatwa tena kwa amri ya kuhamishiwa Arusha, Tanzania, kujibu mashtaka ya mauaji ya kimbari.

Matukio ya hivi punde ambayo yalitokana na ombi la Mahakama Maalum ya Umoja ya Mataifa ya kushughulkikia kesi za Jinai - yanaonekana kuwashangaza wanasheria wake.

Kayishema alikamatwa akiwa katika seli za mahakama kuu mjini Cape Town mapema Jumanne.

Mahakama hiyo inamtaka ajibu mashtaka ya kudaiwa kupanga mauaji ya takriban wakimbizi 2,000 wa Kitutsi katika kanisa katoliki nchini Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Bw Kayishema tayari yuko kizuizini nchini Afrika Kusini baada ya kufuatiliwa katika shamba la mvinyo huko Paarl katika jimbo la Western Cape na awali alikamatwa kwa kukiuka sheria za uhamiaji za nchi hiyo.

Wachunguzi wa Afrika Kusini walisema amekuwa akiishi Afrika Kusini kwa jina la uwongo tangu kuwasili kwake mwaka 2000.

Katika nchi yake ya nyumbani, Rwanda, anashutumiwa kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya 1994, kushiriki katika mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Wakati wa kufikishwa kwake kortini mara ya mwisho mwezi Juni, alitupilia mbali ombi lake la dhamana na akasema angeomba hadhi ya ukimbizi nchini Afrika Kusini.

Kesi dhidi yake imeahirishwa hadi Agosti 30 ili kuruhusu mawakili wake na waendesha mashtaka wa eneo hilo kujibu amri ya kukamatwa na uhamisho.

Hajakubali rasmi mashtaka dhidi yake, lakini hapo awali amekana kuhusika katika uhalifu huo.

Chanzo: Bbc