Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshitakiwa wa mauaji ajifungulia mahakamani

Mimba D Watoto Mshitakiwa wa mauaji ajifungulia mahakamani

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa kike alizaliwa katika Mahakama ya Kithimani, Kaunti ya Machakos nchini kenya baada ya Mama yake ambaye aliyeshtakiwa kwa kosa la mauaji ya Mtoto wake wa miezi 19 kuachiwa huru.

Virginia Mbinya Maingi alikamatwa March 25, 2024, eneo la Kinyaata, Kaunti ya Machakos baada ya kifo cha Mtoto wake ambapo Mahakama iliamuru azuiliwe katika Kituo cha Polisi cha Matuu akisubiri uchunguzi zaidi wa Maafisa wa upelelezi lakini jana Aprili 16 aliachiwa huru na Mahakama baada ya uchunguzi wa kimatibabu kuonesha kuwa Mtoto wake alifariki kutokana na njaa.

Muda mfupi baada ya kuachiliwa huru, Virginia alipata uchungu katika majengo ya Mahakama na kuwafanya Makarani kukimbizana huku na kule kutafuta khanga za kumsitiri ambapo Wauguzi wa Zahanati iliyopo karibu na Mahakama waliitwa haraka kuja Mahakamani na kufanikiwa kumsaidia kujifungua salama mtoto wa kike.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live