Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshirika wa Zuma aunda chama kipya cha siasa Afrika ya Kusini

Mshirika Wa Zuma Aunda Chama Kipya Cha Siasa Afrika Ya Kusini Mshirika wa Zuma aunda chama kipya cha siasa Afrika ya Kusini

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: Voa

Katibu mkuu wa zamani wa chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) Ace Magashule mwenye dosari za ufisadi alizindua chama kipya cha mrengo wa kushoto Jumatano kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.

Magashule mwenye umri wa miaka 63, ni mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma, alifukuzwa kutoka ANC mwaka huu kwa tuhuma za ufisadi lakini bado anapendwa na baadhi ya wapiga kura wanaoegemea mrengo wa kushoto.

"Sisi ni chama kipya cha siasa na tunajiita chama cha watu," Magashule aliuambia mkutano wa waandishi wa habari huko Soweto kuwa kundi jipya linajulikana rasmi kama African Congress for Transformation (ACT).

Hatua hiyo inaweza kupunguza uungwaji mkono zaidi kwa chama cha ANC, wachambuzi wanasema.

Kura za maoni zinaonyesha kuwa kura za chama hicho zinaweza kushuka chini ya asilimia 50 katika uchaguzi wa 2024.

Magashule alisema muundo wake mpya unalenga kupigania hali mbaya ya "Waafrika Kusini wote", na kukitaja chama hicho kuwa makazi mapya ya "wasio na makazi, waliosalitiwa na waliochoka."

ANC "imesonga kwa kasi kuelekea kulia na kuachana na msimamo wake wa kati-kushoto," alisema, akimtetea bosi wake wa zamani, Zuma -- ambaye pia anakabiliwa na tuhuma za ufisadi -- kama muathirika wa mchawi anayesakwa.

"Zuma aliwindwa kama mbwa kwa kupambana na ukiritimba wa kizungu," alisema.

Magashule alisimamishwa kazi kama katibu mkuu wa ANC mwaka 2021 chini ya sera mpya iliyolenga kusafisha sura ya chama hicho baada ya msururu wa kashfa -- na hatimaye kufukuzwa kwenye chama mapema mwaka huu.

Katibu huyo mkuu wa zamani anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi, ulaghai na utakatishaji fedha, kuhusiana na madai ya ubadhirifu wa fedha za umma zilizotengwa kwa ajili ya asbesto kwenye nyumba zilizojengwa na serikali.

Usafishaji huo haukukamilika na wachunguzi wanaamini kuwa sawa na zaidi ya dola milioni 12 ziliwekwa mfukoni.

Chanzo: Voa