Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshauri maalum Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan aonya dalili zote za hatari ya mauaji ya halaiki

Jeshi La Sudan Linasonga Mbele Na Kuuteka Mji Wa Omdurman Mshauri maalum Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan aonya dalili zote za hatari ya mauaji ya halaiki

Wed, 22 May 2024 Chanzo: bbc

Mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya halaiki alionya Jumanne kwamba Sudan inaonyesha dalili zote za hatari ya mauaji ya halaiki, na huenda tayari imeshatekelezwa.

“Ulinzi wa raia nchini Sudan hauwezi kusubiri," Alice Nderitu alisema. "Hatari ya mauaji ya kimbari ipo nchini Sudan. Ni kweli na inakua kila siku."

Nderitu alihutubia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuadhimisha miaka 25 ya azimio kuhusu ulinzi wa raia katika vita vya silaha na maadhimisho ya miaka 75 ya Mikataba ya Geneva.

Alisema raia wengi wa Sudan wanalengwa kulingana na utambulisho wao.

Chanzo: bbc