Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msemaji wa Serikali na Meya wagombana 'Live' kwneye TV

Live Stream Header Msemaji wa Serikali na Meya wagombana 'Live' kwneye TV

Fri, 29 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meya wa mji mkuu wa Uganda, Kampala, siku ya Alhamisi alishambuliana kwa maneno na msemaji wa serikali kwenye kipindi cha TV cha moja kwa moja kabla ya kipindi cha mazungumzo kusimamishwa .

Meya Erias Lukwago, wa chama cha upinzani cha FDC, na msemaji wa serikali Ofwono Opondo walikuwa miongoni mwa wanajopo wanne katika kipindi hicho wakijadili kuhusu uchaguzi mdogo uliomalizika hivi karibuni.

Mjadala huo ulipamba moto na picha zilizosambazwa kwenye Twitter zikamnasa Bw Opondo akimwambia meya "Naweza kukuondoa hapa". Bw Opondo baadaye alisimama huku kukiwa na kurushiana maneno ya hasira kabla ya kipindi hicho kuondolewa hewani.

Kituo cha NBS kilisema wanajopo wote waliondoka studio salama na kuomba radhi kwa watazamaji.

Meya Lukwago alitweet kuwa kilichotokea ni tukio "baya"

"Ombi langu pekee ni kwamba nitoke mahali hapa salama," aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live