Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii Auza Figo Yake Kusaidia Kampeni za Mbunge

Jalango  Na 2mbili 2mbili na Jalang’o

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MSANII maarufu wa Comedy nchini anayefahamika kwa jina la 2mbili, amesema yuko radhi kuuza figo yake ili kumsaidia mtangazi maarufu nchini humo Jalang’o katika kampeni zake za kuwani Ubunge nchini humo.

Jalang’o ambaye jina lake halisi ni Felix Odiwuor amesema wakati akitoa tangazo hilo kupitia kwenye mitandao ya kijamii alikuwa serious na si kwamba alikuwa akifanya mzaha kama baadhi ya watu ambavyo walikuwa wakidhani.

Jalang’o amesema tayari ameshapata mnunuzi wa figo yake; “Wakati niliposema kwamba nauza figo yangu, watu walifikiri nilikuwa nafanya mzaha. Ninataka kuuza figo yangu ili kufadhili kampeni za Jalang’o anayewania ubunge. Tayari nimempata mnunuzi, na nasubiri anitumie hela," 2mbili alisema.

2mbili alisema kwamba figo yake ilipimwa na kupatikana iko sawa na anayehitaji ambapo ameongeza pia kuwa anasubiri alipwe kiwango cha pesa waliokubaliana ili kugharamikia gharama ya upasuaji. 2mbili alisema anapania kuchangia Jalang'o mara nne zaidi ya kile kiwango cha fedha kinachohitajika kufanya kampeni.

“Niliona malengo yake ni kupata zaidi ya Ksh milioni 50, lakini tunataka kutumia zaidi ya Ksh 200 milioni,” alisema 2mbili. Wakati huo huo Wakenya wametoa maoni yao wakidai kwamba Comedian huyo anasaka umaarufu, huku wengine wakitaka awape mawasiliano ya mnunuzi huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live