Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msako mkali dhidi ya jamii ya Tigray unaendelea Ethiopia - UN

Sdasyretrygu Msako mkali dhidi ya jamii ya Tigray unaendelea Ethiopia- UN

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: BBC

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu imesema takriban watu 1,000, wengi wao wakiwa kutoka kabila la Tigray, wamekamatwa tangu serikali ilipotangaza hali ya hatari tarehe 2 Novemba.

Chini ya hali hiyo ya dharura ya miezi sita, serikali ina mamlaka makubwa ya kuwakamata watu, kuwaweka kizuizini washukiwa bila kuwafungulia mashtaka, na kufanya upekuzi nyumbani bila vibali.

Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa alisema "takriban watu 1,000 wanaaminika kuzuiliwa kwa muda wa wiki moja au zaidi - huku ripoti zingine zikiweka idadi hiyo juu zaidi".

Taarifa hiyo ilisema mazingira wanayozuiliwa ni mbaya na wafungwa wengi wanashikiliwa katika vituo vya polisi vilivyo na watu wengi.

Wafanyakazi kumi wa ndani wa Umoja wa Mataifa ambao walikamatwa tarehe 9 Novemba bado wanazuiliwa.

"Wengi wa wale wanaozuiliwa wanaripotiwa kuwa watu wa asili ya Tigray, wanaokamatwa mara kwa mara kwa tuhuma za kuhusishwa au kuunga mkono Tigray People's Liberation Front (TPLF)," UN ilisema.

Katika siku za nyuma, polisi walisema kukamatwa huko hakukuwa na msukumo wa kikabila bali kulilenga wafuasi wa TPLF, ambayo imekuwa ikipambana na serikali kuu tangu mwaka uliopita na sasa wanatishia kuelekea mji mkuu.

Chanzo: BBC