Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msaidizi wa zamani wa Rais wa Congo atoka gerezani

Msaidizi Msaidizi wa zamani wa Rais Congo atoka gerezani

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa msaidizi mkuu wa wafanyakazi wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi, Vital Kamerhe, amerejea nyumbani kwake baada ya kuachiliwa kwa muda.

Msaidizi wake amenukuliwa na vyombo vya habari vya ndani akisema kuwa yuko sawa na aliungana na familia yake.

Bw Kamerhe alipewa uhuru wa muda kwa sababu za kiafya.

Kuachiliwa kwake kulitegemea malipo ya dhamana ya $500,000 (£377,000).

Bw Kamerhe mnamo Juni 20 mwaka jana alihukumiwa kifungo cha miaka 20 ya kazi ngumu na mahakama kuu ya Gombe katika kesi ya ufujaji wa fedha za umma.

Adhabu yake ilipunguzwa kwa kukata rufaa hadi miaka 13 ya kazi ngumu mnamo Juni 2021.

Kamerhe ndio mwanasiasa mkuu zaidi kukabiliwa na kesi ya ufisadi nchini.

Wakili wake alidai kesi hiyo ilikuwa ya kisiasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live