Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msafara wa mwisho wa MINUSMA waondoka Mali

Minusma Un Un.jpeg Msafara wa mwisho wa MINUSMA waondoka Mali

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msafara wa mwisho wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA) umeondoka kwenye kambi yake katika mji wa Tessalit Jumamosi hii, Oktoba 21 mchana.

Utaungana na walinda amani wa mwisho wa Chad kutoka mji wa Aguelok. Makundi hayo mawili yataunda msafara mkubwa kufika Chad kwa njia ya barabara.

Kikosi hicho cha amani cha Umoja wa Matiafa kinachofahamika kama MINUSMA kilitarajiwa kuondoka kutoka kambi zake katikati ya Oktoba lakini kikaahirisha wakati eneo hilo lililopokabiliwa na ongezeko la machafuko na mapigano.

Kwa mujibu wa maafisa wawili wa uwanja wa ndege, jeshi la Mali limetuma ndege mbili katika kambi ya Tessalit zikiwabeba vikosi vya wanajeshi na wapiganaji wa kundi la mamluki la Wagner kutoka Urusi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live