Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msafara wa kwanza wa wanajeshi wa Ufaransa umewasili Chad

Msafara Wanajeshi Chad Kufika.png Msafara wa kwanza wa wanajeshi wa Ufaransa umewasili Chad

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msafara wa kwanza wa wanajeshi wa Ufaransa wanaondoka nchini Niger, umewasili nchini Chad, jeshi la Ufaransa limethibitisha.

Kwa mujibu wa kanali Pierre Gaudilliere, msafara huo umewasili katika mji mkuu wa Chad N’Djamena baada ya siku tisa ukiwa barabarani.

Wanajeshi hao wanatarajiwa kuondoka tena nchini Chad wakielekea nchini Ufransa kwa kutumia usafiri wa angani.

Kwa mujibu wa Gaudilliere, safari hiyo ya njia ya barabarani ilikuwa imefanikishwa kwa usaidizi wa wanajeshi wa Niger.

Ufaransa ilianza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger wiki iliyopita baada ya kuangushwa kwa utawala wa rais Mohamed Bazoum mwezi Julai, kiongozi huyo alikuwa mshirika wa karibu wa Ufaransa na mikakati yake katika ukanda wa Sahel.

Karibia wanajeshi wa 1,400 wa Ufaransa walikuwa jijini Niamey na eneo la Magharibi mwa Niger katika juhudi za kupambana na makundi ya kijihadi ambapo walikuwa wakitumia silaha za kisasa ikiwemo ndege za kivita, helikopta na magari ya kivita pamoja na sila nyengine.

Msafara huo umewasili nchini Chad kwa kutumia usafiri wa barabara ambapo wamesafiri zaidi ya kilomita 1,600 wakisindikizwa na wenzao wa Niger.

Mji mkuu wa Chad N'Djamena ni makao makuu ya wanajeshi wa Ufaransa katika eneo pana la Sahel, karibia wanajeshi elfu moja wakiwa huko.

Jumatano ya wiki hii, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikuwa mwenyeji wa rais wa Chad Mahamat Idriss Deby kwa mazungumzo katika Ikulu ya Elysee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live