Msafara wa kiongozi wa Muungano wa Azimio Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga siku ya Jumatatu ulijitokeza kupitia eneo la Kawangware jijini Nairobi ili kuendeleza maandamano ya pili dhidi ya serikali .
Odinga aliambatana na naibu wake katika Muungano wa huo Martha Karua , kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na kiongozi wa chama cha Roots Party George Wajackoyah, miongoni mwa viongozi wengine wa upinzani.
Dakika chache baada ya kuanzisha maandamno hayo huku msafara wa kiongozi huyo ukipenya katika makazi hayo , maafisa wa polisi waliwarushia vitoa machozi waandamanajiwaliokuwa wakibeba matawi ya miti , mabango , sufuria ,na baadhi ya vyakula ili kupinga hali ya juu ya Maisha.
Hatua hii inajiri baada ya Inspekta mkuu wa Polisi IGP kudai kwamba maandamano hayo yalikuwa haramu.