Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msaada zaidi unahitajika kwa dharura mashariki mwa DR Congo - MSF

Msaada Zaidi Unahitajika Kwa Dharura Mashariki Mwa DR Congo   MSF Msaada zaidi unahitajika kwa dharura mashariki mwa DR Congo - MSF

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Shirika la madaktari wasio na mipaka, Médecins Sans Frontières, limesema msaada zaidi wa kibinadamu unahitajika kwa dharura mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

MSF imesema takribani watu milioni moja wamelazimika kukimbia makazi yao katika jimbo la Kivu Kaskazini katika kipindi cha mwaka jana kutokana na mapigano makali yanayohusishwa na kundi la waasi la M23.

Shirika hilo limesema wengi wa waliokimbia makazi yao wanaishi katika hali mbaya na timu zake zimezidiwa kabisa na ongezeko la visa vya surua na kipindupindu.

Nchi kadhaa za Afrika Mashariki zimetuma wanajeshi mashariki mwa Congo katika juhudi za kuwataka waasi wa M23 kuondoka.

DR Congo imeishutumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuunga mkono kundi la waasi, madai ambayo Kigali inakanusha.

Chanzo: Bbc