Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mripuko mkubwa watikisa uwanja wa ndege Sudan

Karthouom Sudan Mripuko mkubwa watikisa uwanja wa ndege Sudan

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mripuko mkubwa uliutikisa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mji mkuu wa Sudan Khartoum jana Jumamosi huku kukiwa na taarifa zinazokinzana kuhusu sababu za mripuko huo.

Moto na moshi mzito ulionekana ukipanda hewanni katika eneo la katikati mwa Khartoum. Eneo hilo llina taasisi muhimu kama vile uwanja wa ndege, ikulu ya rais, na Kamandi Kuu wa Kikosi cha Wanajeshi wa Sudan (SAF).

Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa jina lake, amesema kuwa mripuko huo umetokea katika ghala la mafuta ya ndege ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum baada ya kutoikea moto kutokea kwenye eneo hilo. Lakini mtu mwingine aliyeshuhudia amesema umetokea karibu na ikulu ya rais katikati ya mji mkuu huo.

Mapigano kati ya Jeshi la Sudan, SAF na Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF) yaliendelea jana Jumamosi katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu, Khartoum.

Vita baina ya majenerali wa kijeshi vimeisababishia Sudan madhara makubwa

Jeshi la Sudan jana lilishambulia vituo kadhaa vya RSF huko kusini mwa Khartoum, kwa kutumia ndege za kivita na makombora ya kivita.

Sudan imekuwa ikishuhudia mapigano makali ya silaha kati ya SAF na RSF tangu Aprili 15. Ripoti za Wizara ya Afya ya Sudan zinasema kuwa mapigano hayo yameshapelekea zaidi ya watu 3,000 kuuawa na zaidi ya 6,000 kujeruhiwa.

Zaidi ya watu milioni 4 wamekimbia makazi yao, huku milioni 3.2 wakiwa ni wakimbizi wa ndani ya Sudan na karibu 900,000 wakikimbilia katika nchi jirani za Chad, Misri, Sudan Kusini na nchi nyinginezo. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live