Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrembo wa Kenya adaiwa kudukua mfumo na kuiba bilioni 280 Zimbabwe

Primrose Nyeri Mwangi.jpeg Primrose Nyeri Mwangi

Thu, 12 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja raia wa Kenya anakabiliwa na mashitaka ya ulaghai nchini Zimbabwe baada ya kudaiwa kuhusika katika udukuzi wa mifumo ya Mfuko wa Maendeleo ya Wafanyakazi wa Zimbabwe (ZIMDEF) na kuhamisha dola milioni 120 (TZS bilioni 280) kutoka kwenye akaunti ya benki ya wakala wa serikali.

Primrose Nyeri Mwangi (40) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Primkett Travel and Tours and Mafkett Trading, anadaiwa kushirikiana na watu wengine wawili kudukua mifumo ya data ya ZIMDEF ambapo walipata 'codes' za kuiba pesa kutoka kwenye akaunti za shirika hilo.

Aidha, washitakiwa hao pia wanadaiwa kuhamisha fedha nyingine katika akaunti ya Atrier Engineering CBZ, Newplaces (Pvt) Limited akaunti ya NBS na akaunti ya Tavaka Holding NBS.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live