Mwanamke raia wa Kenya anayejulikana kwa jina la Brendalicious kwenye Instagram amefariki dunia nchini Malaysia akidaiwa kuwa alikuwa akisafirisha dawa za kulevya.
Marehemu aliyejulikana kwa jina la Brenda alifika katika uwanja wa ndege wa Malaysia na kuanza ‘kufanya mambo ya ajabu ili kuwavutia walinzi’.
Kisha akaanguka chini na kuanza kutetemeka na kutoa povu mdomoni, inaonekana, mfuko mmoja wa kokeini aliokuwa amebeba tumboni ulikuwa umepasuka.
Alikimbizwa katika hospitali moja nchini Malaysia ambako alifariki alipokuwa akipatiwa matibabu. Madaktari wa uchunguzi walipochunguza mwili huo, walipata vidonge 34 vya kokeini tumboni mwake.
Enzi za uhai wake kupitia ukurasa wake wa Instagram, mrembo huyo ameonekana akiishi maisha ghali na ya kuvutia huku akijielezea kama ni mwanafunzi aliyekuwa akisomea sheria.