Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrembo Aliyetabiri Kifo Chake Afariki Dunia

Uthibitisho Wa Ukiukwaji Wa Haki Za Binadamu Sudan Kusini Mrembo Aliyetabiri Kifo Chake Afariki Dunia

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Cleo Maina, mwanadada kutoka nchini Kenya aliyejitabiria kifo kuwa angekufa Desemba 29, 2021 yametimia kweli kama alivyosema baada ya kuaga dunia.

Maina alichapisha ujumbe wa kuzua wasiwasi kwenye ukurasa wake wa Twitter ulionyesha kuwa mambo hayakuwa sawa "Sehemu ya safari ni mwisho…," aliandika. Siku chache baadaye, kifo chake kilitangazwa na mwanahabari Oliver Mathenge ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu.

Watu wengi ambao wanamfahamu wamejitokeza kwa wingi kwenye Twitter kumuombolezea Cleo wakimtaja kama mtu aliyekuwa mchangamfu na mwingi wa furaha. Mathenge alimuelezea marehemu kama mtu mwema ambaye walifurahia wakati wao pamoja.

"Uliona bora kwangu kila wakati hata nisingeweza! Ulisherehekea ushindi wangu kama ni wa kwako mwenyewe. Tulishiriki nyakati za ajabu. Wakati mwingine tulilia. Mtu wa karibu sana. Nitakusherehekea kila wakati, Cleo," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live