Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrembo Akinukisha "Barabara Mbovu Imenizuia Kupata Mume"

Mrembo Barabara Mrembo huyo akilalamika.

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MREMBO mmoja amelalamika kuwa barabara mbovu inayounganisha jamii kadhaa katika eneo lake imemzuia kupata mume akidai kwamba wanaume ambao wanatakiwa kuoa wanawake wa hadhi yake, huvamiwa kila wakati na watu wapya hawawezi kuingia katika jamii yake sababu ya barabara mbovu.

Tovuti ya habari ya Nigeria, Legit.ng iliposti maoni ya wanamitandao kuhusu malalamiko ya mrembo huyo nchini Ghana amelalamikia namna anavyohangaika kupata mume sababu ya barabara mbovu inayounganisha jamii katika eneo lake.

Katika video ambayo imewavunja mbavu watumiaji wa mitandao, mrembo huyo alihoji kuwa wakati mwingine wageni wanapoingia katika mji wake na kutaka kutumia barabara yao, huwa wanakata tamaa na kurudi walikotoka.

Isitoshe, mrembo huyo ambaye hakujitambulisha wala jamii yake, alidai kuwa visa vya wizi wa kutumia nguvu vimekithiri sana eneo hilo na kuibia wanaume mali ambayo wangelitumia kuoa wanawake wa kaliba yake.

"Jinsi barabara ilivyo mbovu, majambazi wanaendelea kuwaibia wanaume ambao wangetaka kutuoa. Hivyo tunaiomba serikali ije kututengenezea barabara ili tupate mapenzi," aliongeza.

Maoni ya wanamtandao

Priscilla Vidza alisema: "Dereva mmoja wa teksi aliniambia angelikuwa ni mpenzi wangu angeachana nami kwa sababu ya hali mbaya ya barabara yangu oo."

Fx Amoah alihoji: "Nyinyi nyote kuamka alfajiri kupanga misururu mirefu ya kuwapigia kura wanasiasa na kushangilia mtaani wakati mwakilishi wa chama chenu anaposhinda bila kujali anafanya kazi hiyo au anahitaji ofisi tu kwa ubadhirifu wa fedha."

Asiedu Lawrencia: "Inaweza kuwaukweli kwa sababu niliwahi kumuona bi wa mjini na baba yangu akiuliza kama atakuja hapa barabara ya kuelekea mjini hmmmm bado nawaza jibu naenda kumpa."

Nutsu GH alisema: "Eric Abaidoo nadhani itakuwa fursa nzuri ya utafiti kuchunguza athari za barabara mbaya kwenye matokeo ya baadaye ya ndoa ya wanawake katika jamii hii."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live