Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrembo Afanyiwa Shambulio na Nyuki, Ushirikina Watajwa

Newslite1635500236460 Mrembo huyo

Fri, 29 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TUKIO la kushangaza limetokea eneo la Machakos Mjini, Kaunti ya Kitui nchini Kenya ambapo kundi kubwa la nyuki limemvamia mwanamke mmoja mudA mfupi tu baada ya kutoka kwenye bajaji juzi, Jumatano, Oktoba 27, 2021.

Katika picha zilizosambaa mitandaoni, nyuki hao wanaokana wakiwa wamejaa kwenye mkono wa kulia wa mrembo huyo.

Imeripotiwa kuwa polisi walijaribu kuwaondoa nyuki hao lakini juhudi zao hazikufua dafu. Umati mkubwa wa watu ulikusanyika katika eneo la tukio kujionea maajabu wengi wakisema yalitokana na uchawi. Baadaye mwanamke huyo aliondolewa katika eneo la tukio na dereva mmoja ambaye hakutambuliwa na kutoweka kusikojulikana.

Hali hiyo iliwafanya wengi kushuku kuwa walikuwa pamoja huku wengine wakisema mkoba aliokuwa amebeba mrembo huyo ulikuwa umejaa pesa na ndiyo maana nyuki hao walitumwa kumlinda asipokonywe. Baadhi nao walidai kuwa mkoba huo ulikuwa na mali ya wizi zikiwemo nguo na pesa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live