Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpox: DRC kupokea dozi za kwanza za chanjo wiki ijayo

Homa Ya Nyani Mpox: DRC kupokea dozi za kwanza za chanjo wiki ijayo

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inatarajia kupokea dozi za kwanza za chanjo dhidi ya mlipuko wa Homa ya Mpox wiki ijayo katika nchi hii ambapo ugonjwa huo tayari umeua takriban watu 570, Waziri wa Afya amesema.

DRC ambayo iliyoathiriwa zaidi, imerekodi wagonjwa 16,700, "na zaidi ya watu 570 wamefariki" tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Waziri Samuel-Roger Kamba amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

"Tuna nchi mbili kimsingi ambazo zimetuahidi chanjo. Nchi ya kwanza ni Japani. Na nchi ya pili ni Marekani," amesema.

Marekani imeahidi dozi 50,000, wakati "Japani ilitia saini asubuhi ya leo (Jumatatu) na mamlaka kwa dozi milioni 3.5, kwa ajili ya watoto pekee," alieleza mkuu wa kitengo cha kukabiliana na mlipuko huo ambaye hakutaka jina lake litajwe.

DRC nchi yenye wakazi wapatao milioni mia moja "inakusudia kuchanja watu milioni 4 wakiwemo watoto milioni 3.5," kliongeza chanzo hiki.

"Ninatumai kuwa wiki ijayo, tutaweza kuona chanjo zikiwasili (...) Mpango wetu wa kimkakati wa kukabiliana na chanjo tayari uko tayari, tunasubiri tu chanjo zifike," amebainisha Waziri wa Afya.

Ugonjwa huo "unaathiri vijana zaidi na zaidi na tuna watoto wengi walio na umri wa chini ya miaka kumi na tano ambao wameathirika," amesema.

Mlipuko wa sasa una virusi vinavyoambukiza zaidi na hatari, na kiwango cha vifo kinachokadiriwa cha 3.6%.

Kuibuka tena kwa homa ya Mpox nchini DRC, ambayo pia inaathiri Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda, kulisukuma Shirika la Afya Duniani (WHO) kuanzisha kiwango chake cha juu cha tahadhari katika ngazi ya kimataifa siku ya Jumatano.

DRC ndio kitovu cha mlipuko wa sasa, kuenea kwa aina hatari zaidi ya virusi vinavyosababisha wasiwasi unaokua barani Afrika na kwingineko.

Nje ya Afrika, kesi za Mpox zimegunduliwa nchini Sweden, Pakistani na Ufilipino.

Virusi hivyo vilivyoitwa Monkeypox viligunduliwa mwaka wa 1958 huko Denmark, katika tumbili waliofugwa kwa ajili ya utafiti. Kisha mwaka 1970 kwa mara ya kwanza kwa binadamu katika nchi ambayo sasa ni DRC (zamani Zaire).

Mpox ni ugonjwa wa virusi ambao huenea kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu lakini pia hupitishwa kupitia mawasiliano ya karibu ya mwili. Ugonjwa huo husababisha homa, maumivu ya misuli na vidonda vya ngozi.

"Msile nyama ya mnyama aliyekufa, msiguse wanyama wagonjwa, kwa sababu pia ni njia ya kuambukizwa," amesema Waziri Kamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live