Chama cha Citizens Coalition for Change, CCC kimesema mwanaharakati huyo aliingizwa kwenye gari na watu wasiojulikana wakati alipokuwa akishiriki shughuli ya kampeini ya mgombea wa chama hicho kabla ya uchaguzi ujao wa marudio utakaofanyika Desemba 9.
Msemaji wa chama hicho Promise Mkwananzi amesema mwanaharakati huyo aliiteswa na kisha kutupwa nje ya mji mkuu Harare.Hata hivyo shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha juu ya tukio hilo.
Kutekwa nyara na kuuwawa kwa Masaya kumetokea katika kipindi cha takriban wiki mbili baada ya tukio jingine, la kutekwa, kuteswa,na kisha kutupwa,na watu waliokuwa na silaha, mwanasheria Takudzwa Ngadiore.
Zimbabwe ina historia ya muda mrefu ya matukio kama hayo ya kuuwawa kwa wanaharakati wa kisiasa na Upinzani mara nyingi umekuwa ukituhumu,yanafanywa na chama tawala cha Zanu PF.