Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpelelezi wa tukio la ubakaji Afrika Kusini afariki dunia

Mpelelezi Wa Tukio La Ubakaji Afrika Kusini Afariki Dunia Mpelelezi wa tukio la ubakaji Afrika Kusini afariki dunia

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Polisi nchini Afrika Kusini wamethibitisha kifo cha mmoja wa wapelelezi wakuu katika tukio la kutoroka jela kwa muhalifu wa ubakaji na mauaji Thabo Bester.

Polisi walisema wanachunguza mazingira ya tukio hilo la kujiua kwa Brigedia Jackson Mkhaulesi mwenye umri wa miaka 59. Alipatikana amefariki ndani ya gari lake siku ya Jumatatu.

Mapema siku hiyo, alihudhuria kikao cha mahakama ambapo mpenzi wa Bester, daktari maarufu Nandipha Magudumana, alishindwa ombi lake la kutangaza kukamatwa kwake nchini Tanzania kwamba ilikuwa kinyume cha sheria.

Habari za kifo cha Brigedia Mkhaulesi zimeleta mshtuko nchini Afrika Kusini. Afisa wa upelelezi wa polisi aliyehudumu kwa miaka 31 ametajwa kuwa afisa mchapakazi na mwaminifu.

Bester anajulikana kama "mbakaji wa Facebook" kwa kutumia tovuti za mitandao ya kijamii kuwarubuni waathiriwa wake. Alidanganya kufariki na kutoroka gerezani mwaka jana. Yeye na mpenzi wake, ambaye anatuhumiwa kumsaidia kutoroka, walikamatwa nchini Tanzania mwezi Aprili na kurejeshwa Afrika Kusini ili kujibu mashtaka.

Chanzo: Bbc