Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango wangu ni kumshinda DP Ruto mwaka ujao, Kalonzo asema

Bcca59b5d7988ca4 Mpango wangu ni kumshinda DP Ruto mwaka ujao, Kalonzo asema

Mon, 26 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mikutano ya Kalonzo na Raila Odinga imekuwa ikizua ripoti za wawili hao kuwa kwenye mazungumzo ya kufufua muungano wao ili wawanie urais 2022Hilo limekuwa likizua shauku dhidi ya wandani wa Kalonzo kwenye muungano wa One Kenya AllianceKalonzo hata hivyo anasema hilo haliwezekani kwani mpango wake ni kuwania urais ili aweze kumbwagwa DP RutoKiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amepuuza madai kuwa anapanga kuungana na kinara wa ODM Raila Odinga kwenye siasa za 2022.

Akiongea Mwingi Jumamosi Julai 24, Kalonzo alisema mikutano yake na Raila imekuwa na kudai fedha za vyama ambapo ODM ilipokea kwa niaba ya muungano wa NASA.

"Nimeona magazeyti leo yakisema eti mimi na Raila tuliketi, mimi ni mtu mwenye uwazi na wenzangu Musalia Mudavadi na Wetangula wanajua mimi ninaketi na Raila kudai mgao wa fedha za vyama," alisema Raila.

Kiongozi huyo wa Wiper alisema yeye yuko kwenye mbio za kuingia Ikulu katika uchaguzi mkuu ujao na hawezi kuwa mgombea mwenza wa mtu.



Read also

Hisia Mseto Baada ya Kalonzo Musyoka Kukutana na Muthama



Alisema kwa sasa anaangazia vile atafaulu kukabiliana na Naibu Rais William Ruto kwenye uchaguzi huo.

"Kwa sasa mimi naangazia vile nitamshinda William Ruto mwaka ujao, hilo ndilo muhimu kwangu sasa," alisema Kalonzo.

Kiongozi huyo wa Wiper alisema wanasiasa pia waruhusiwe kuzuru kila kona ya nchi kuomba kura pasi baadhi ya maeneo kutajwa kama ngome ya vigogo fulani.

DP Ruto amekuwa akiwatania Kalonzo na wenzake kwenye uliokuwa muungano wa NASA akisema yuko tayari kukabiliana na wao.

"Ukiona hao sasa wanatapatapa hawajui ni huyu ama ni yule jua kimeumana," alisema DP kuhusu vigogo wa NASA.

Ruto alisema kile Kalonzo, Raila, Musalia, Wetangula na Moi wanasubiri ni kuungwa mkono na Rais Uhuru Kenyatta.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke