Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango wa wahamiaji Rwanda waungwa mkono na wabunge Uingereza

Rishi Sunak Mpango wa wahamiaji Rwanda waungwa mkono na wabunge Uingereza

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, Jumanne, Disemba 12, amefanikiwa kumaliza uasi uliokuwa ndani ya chama chake cha Conservative, kwa kupata uungwaji mkono wa wabunge kuhusu mpango wake wa kuwatuma wahamiaji nchini Rwanda.

Wabunge 313 walipiga kura kuunga mkono muswada huo unaoitwa usalama wa Rwanda, huu ukiwa ni ushindi wa kwanza wa kesi hiyo.

Ni muswada mpya ulioundwa kushughulikia maswala yaliyotolewa na Mahakama ya Juu ya Uingereza, ambayo mwezi uliopita ilitangaza sera hiyo kuwa kinyume cha sheria.

Muswada huu utazilasimisha mahakama za nchi hiyo kuiona Rwanda kama nchi salama, huku pia ukiondoa nafasi yoyote ya waomba hifadhi kufungua kesi kupinga kufukuzwa kwenye taifa hilo.

Matokeo ya kura hii yamekuwa ni ushindi wa kwanza mkubwa wa waziri mkuu Sunak, ambaye tangu ameingia madarakani, aliweka ajenda ya kushughulikia uhamiaji haramu kama kipaumbele.

Hata hivyo licha ya kupata uungwaji mkono, huenda mwakani akalazimika kufanya marekebisho katika baadhi ya vipengele vya mkataba huo, ambavyo watetezi wa haki za binadamu wameonya vinaenda kinyume na sheria za kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live