Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango wa kubinafsishaji Shirika la Ndege la Afrika Kusini waporomoka

Mpango Wa Kubinafsishaji Shirika La Ndege La Afrika Kusini Waporomoka Mpango wa kubinafsishaji Shirika la Ndege la Afrika Kusini waporomoka

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Afrika Kusini imesitisha mkataba wa kuuza hisa katika shirika lake la ndege la taifa baada ya kushindwa kuafikiana kuhusu thamani na masharti mengine na muungano wa wawekezaji binafsi.

Serikali tangu mwaka 2021 ilikuwa imepanga kuuza asilimia 51 ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lililopata hasara kwa Muungano wa Takatso, kama sehemu ya juhudi za kukomesha uokoaji wa mara kwa mara wa ndege hiyo.

Baada ya miaka mitatu ya mazungumzo, Waziri wa Mashirika ya Umma Pravin Gordhan Jumatano alisema makubaliano hayo yamekatishwa "kwa kuwa hakuna njia wazi ya kusonga mbele".

Bw Gordhan alitaja athari za soko la baada ya Covid-19 kama jambo muhimu katika uamuzi huo.

"Tuna hakika kwamba SAA inaweza kujiendeleza katika mwaka ujao hadi miezi 18 na kwamba kuna njia nyingine mbalimbali ambazo ufadhili wa haraka unaweza kupatikana," aliongeza.

Katika taarifa, Muungano wa Takatso ulisema mabadiliko ya mkataba wa kununua SAA yangechukua muda mrefu sana kuafikiwa.

SAA sasa itarejea kuwa ya serikali kikamilifu lakini serikali ilisema shirika hilo la ndege liko tayari kuingia katika ushirikiano mwingine.

Kuporomoka kwa makubaliano hayo ni pigo kwa juhudi za Rais Cyril Ramaphosa za kuuza vyombo vya dola visivyofanya kazi vizuri na kudhibiti deni la serikali.

Chanzo: Bbc