Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpaka wa Afrika Kusini na Zimbabwe wafungwa

Zim Sa Pic Mpaka wa Afrika Kusini na Zimbabwe wafungwa

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Barabara inayounganisha nchi za Afrika Kusini na Zimbabwe imefungwa katika mpaka wa Beitbridge ikiwa ni mara ya pili kufungwa kwa mwaka 2021.

Foleni kubwa ya magari imeshuhudiwa ikiwa na umbali wa zaidi ya Km 20 kutoka mpaka wa Mto Limpopo uliopo Afrika Kusini hadi mji wa Musina nchini humo.

Inaelezwa kuwa magari mengi yaliyokwama mpakani hapo ni malori ya mizigo yaliyobeba bidhaa zinazoelekea nchini Zimbabwe, Zambia, Malawi na Tanzania.

Madereva wametakiwa kubaki na magari yao huku wengi wao wakiwa eneo hilo kwa zaidi ya wiki moja sasa. Bado hawajui hatma yao kwani hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Mamlaka za nchini Afrika Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live