Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto wazuka katika kanisa la Nabii T B Joshua wakati wa ibada ya wafu

C3b38276f7313710 Moto wazuka katika kanisa la Nabii T B Joshua wakati wa ibada ya wafu

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Moto ulizuka katika kanisa la nabii marehemu T B Joshua la Synagogue Church Jumatatu, Julai 5, 2021Waombolezaji walikimbilia usalama wao, hakuna aliyejeruhiwa kwenye mkasa huo ambao unasemekana kusababishwa na hitilafu ya umemeNabii Joshua atazikwa Ijumaa, Julai 9 katika kanisa lake kama alivyopendekeza kabla ya kifo chakeMoto mkubwa ulizuka katika kanisa la Synagogue Church of Nations usiku wa Jumatatu, Julai 5 wakati wa ibada ya kumpa heshima za mwisho mwendazake Nabii T B Joshua.

Kwa mujibu wa taarifa za Nation, viongozi wa kanisa hilo walisema kwamba mkasa huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme lakini uliweza kudhibitiwa kwa haraka.

Waombolezaji walikimbilia usalama wao huku ibada ikikatizwa, hakuna aliyejeruhiwa kwenye mkasa huo.

" Siku ya Jumatatu, Julai 5, 2021, kulizuka moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme uliotokea kwenye ghala la kanisa la Synagogue Church of All Nations," Taarifa kutoka kwa viongozi wa kanisa hilo walisema.

Mkewe marehemu nabii T B Joshua Evelyn Joshua ndiye amekuwa akiongoza waombolezaji katika ya ibada ya kila siku tangu kifo cha mumewe.

" Tunashukuru Mungu kwamba hakuna majeruhi na tunawahakikishia waomboleza usalama tunapoendelea kumkumbuka na kumpa heshima za mwisho nabii T B Joshua," Taarifa hiyo iliongezea.

Nabii TB Joshua alifariki dunia Juni 5,2021 siku chache kabla ya kuadhimisha miaka 58 tangu kuzaliwa kwake.

Kama alivyopendekeza, marehemu Nabii Joshua atazikwa karibu na kanisa lake siku ya Ijumaa, Julai 9 mjini Lagos, Nigeria.

Awali taarifa kutoka kwa usimamizi wa kanisa hilo ilisema kwamba waumini watakuwa na ibada kila siku kwa wiki moja ya maombolezo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke