Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto wazuka kambi ya polisi

Polisi Motoo Moto wazuka kambi ya polisi

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ajali ya Moto imetokea katika kambi ya Polisi nchini Misri na bado haijajulikana chanzo cha moto huo.

Ajali hiyo imetokea leo Alfajiri nchini humo katika Mji wa Ismailia na hakuna mtu aliyepoteza maisha.

Idara ya Usalama jijini humo imesema Video zilizotapakaa kwenye mitandao ya kijamii zimeonesha miali ya moto ikiongezeka na ilionekana kuwa sehemu kuu ya jengo hilo ilikuwa imeporomoka.

Mashahidi wawili waliliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa vyombo vya moto vilitumwa kwenye eneo la tukio, lakini vilionekana kujitahidi kuuzuia moto huo.

Baadhi ya watu walionekana wakitolewa nje lakini haikufahamika iwapo kulikuwa na majeruhi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live