Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto wateketeza sehemu ya Mlima Longonot Kenya

Mlima Moto Sehemu Kenya Moto wateketeza sehemu ya Mlima Longonot Kenya

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: BBC

Mlipuko wa moto umeteketeza hekta za misitu katika Mlima Longonot nchini Kenya, ambao ni kivutio maarufu kwa wasafiri katika eneo la Bonde la Ufa.

Shirika la Huduma ya Wanyamapori nchini (KWS) linasema kwenye taarifa kwamba lilizima moto huo ulioanza Alhamisi.

KWS ilikanusha uvumi unaoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kumekuwa na mlipuko wa volcano, na kusema ilitaka "kuhakikisha kuwa mbuga hiyo iko salama kwa wageni wote".

Mlima huo ambao ni volcano iliyotulia, imekuwa moja ya mada zinazozungumzwa sana kwenye mtandao wa Twitter, huku baadhi ya watumiaji wakidai kuwa walikumbana na tetemeko la ardhi kutokana na mlipuko huo unaodhaniwa kuwa

Chanzo cha moto huo kwenye mlima bado hakijajulikana. Mwaka jana, mlipuko kama huo wa moto ulipunguza sehemu ya mimea katika mbuga hiyo kuwa majivu

Chanzo: BBC